Matthew 13:13-15

13 aHii ndiyo sababu nasema nao kwa mifano: “Ingawa wanatazama, hawaoni;
wanasikiliza, lakini hawasikii, wala hawaelewi.

14 bKwao unatimia ule unabii wa Isaya aliposema: “ ‘Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa;
na pia mtatazama lakini hamtaona.

15 cKwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu;
hawasikii kwa masikio yao,
na wamefumba macho yao.
Wasije wakaona kwa macho yao,
na wakasikiliza kwa masikio yao,
wakaelewa kwa mioyo yao,
na kugeuka nami nikawaponya.’

Copyright information for SwhKC